1.6 Masharti ya kutumia Huduma za Utengamao Kidijitali

Kwa ujumla katika utengamao, Huduma za Utengamao Kidijitali zinaweza kutumika kwa wateja wote. Hata hivyo, kama mifano inavyoonyesha hapo juu, baadhi ya vipengele vinaweza kuzuia utekelezaji wa Huduma za Utengamao Kidijitali. Katika sehemu hii tungependa kutaja vipengele vinavyopaswa kuzingatiwa na kutumika kama masharti ya utekelezaji wa Huduma za Utengamao Kidijitali.

Kabla ya kujadili masharti ambayo yanaathiri wateja, wataalamu wa huduma za utengamao na jamii, tungependa kuwasilisha baadhi ya vipengele vya jumla ambavyo ni muhimu wakati ambapo teknolojia za kidijitali zinaunganishwa katika huduma za utengamao.

1.6.1 Masharti ya Jumla

  • Moja ya masharti ya mchakato wa huduma za utengamao wenye mafanikio ni urahisishaji wa huduma ili kukidhi mahitaji ya kibinafsi ya mteja. Hii ina maana kwamba utekelezaji wa Huduma za Utengamao Kidijitali lazima uhusishe na ujumuishe lengo na matumaini ya mteja. 
  • Aidha, uingiliaji kati wa ana kwa ana hubadilishwa na vipengele vya kidigitali pekee kwa kiasi. Hii ina maana kwamba kuna tiba iliyochanganywa, ambapo ina maana ya kuingiliana kwa vipengele vya kidijitali.
  • Masharti ambayo yanafaa kuzingatiwa yanategemea pia teknolojia tofauti zinazotumika. Hatuonyeshi masharti kwa kila teknolojia, lakini tunakupa maelezo ya jumla.
  • Masharti yaliyo hapa chini hayapaswi kuzingatiwa peke yake lakini kwa ujumla. Yanaweza kutenganishwa mara chache kutoka kwa kila moja na hivyo basi yanapaswa kuzingatiwa.

1.6.2 Masharti kwa wateja 

Masharti yafuatayo yanapaswa kujadiliwa na mteja kabla ya Huduma za utengamao Kidijitali kutekelezwa. Vipengele hivi vinapaswa kumsaidia mtaalamu wa huduma za utengamao kuweka Huduma za Utengamao Kidijitali wa kibinafsi ambapo mwingiliano wa ana kwa ana na mtaalamu wa huduma za utengamao hujumuishwa katika programu ya kidijitali ili kuwezesha vikao vya kidijitali. Majadiliano ya mambo haya huwezesha kutoa mwelekeo unaofaa wa Huduma za Utengamao Kidijitali kwa mteja binafsi na kukuza ufikiaji wa malengo yao na, kutoa uamuzi wa kiwango kinachofaa cha mwongozo wa matibabu pamoja na matumizi ya kidijitali. Vipengee vyote vinaonyeshwa na mifano. Vipengele vifuatavyo vimepatikana kutoka [34].

Motisha na idhini ya mteja

Mfano: Je, mteja ana nia ya kutumia Huduma za Utengamao Kidijitali? Fikiria mtazamo wa mteja kuhusu teknolojia ya dijitali, uzoefu wa awali na Huduma za Utengamao Kidijitali, imani kuhusu manufaa ya teknolojia ya dijitali.

Teknolojia 

Mfano: Je, mteja anaweza kufikia teknolojia inayohitajika ili kutekeleza Huduma za Utengamao Kidijitali? Fikiria upatikanaji wa mtandao, simu janja, au kitarakilishi. 

Nafasi 

Mfano: Je, mteja ana nafasi ya kutosha ya kutekeleza Huduma za Utengamao Kidijitali? Fikiria ikiwa mteja ana pahali palipo kimya, faraghani, pahali tulivu pa huduma za utengamao, na kuzingatia kuwa baadhi ya teknolojia za dijitali zinahitaji nafasi fulani.

Usalama

Mfano: Je, usalama wa mteja unahakikishwa wakati wa huduma za utengamao unatekelezwa bila kuwepo kwa mtaalamu wa tiba? Fikiria hali ya kimwili na kiakili au uwezekano wa kupingana.

Ujuzi wa kompyuta 

Mfano: Je, inawezekana kwa mteja kujifunza jinsi ya kutumia teknolojia ya dijitali inayohitajika? Fikiria utendaji wa teknolojia ya dijitali.

Ujuzi wa (afya) dijitali

Mfano: Je, mteja anaweza kufasiri maandiko, video, na/au faili za sauti kama zilivyowasilishwa katika teknolojia ya dijitali? Fikiria kiwango cha ujuzi wa mteja wa dijitali(afya), lugha, na utambuzi.

1.6.3 Masharti kwa wataalamu wa utengamao

Vipengele vifuatavyo vinapaswa kuonyeshwa na mtaalamu wa huduma za utengamao na kisha kuamua kama vinafaa katika Huduma za Utengamao Kidijitali. Kila hitaji linaelezewa kwa kutumia mfano. Vipengele vifuatavyo vinahusishwa na [34,35].

Teknolojia

Mfano: Je, mtaalamu wa huduma za utengamao ana uwezo wa kufikia teknolojia inayohitajika ili kufanya Huduma za Utengamao Kidijitali? Fikiria ufikiaji wa mtandao, simu janja, vitarakilishi au kompyuta, na programu zote zinazohitajika ili kutoa huduma. Kamera tofauti na kongamanosimu/vipokea sauti vinavyobanwa kichwani vinaweza kuhitajika pia ili kuongeza ubora wa video au sauti inayohamishwa kwa mteja.

Nafasi

Mfano: Je, mtaalamu wa afya ana nafasi ifaayo ya kutoa Huduma za Utengamao Kidijitali? Fikiria kwamba wataalamu wa huduma za utengamao wanahitaji pahali palipo kimya, faraghani, pahali tulivu pa huduma za utengamao, na kuzingatia kuwa baadhi ya teknoloji za dijitali zinahitaji nafasi fulani.

Ujuzi wa kompyuta

Mfano: Je, mtaalamu wa huduma za utengamao anafanya kazi kwa kutumia teknolojia za kidijitali? Fikiria utendakazi wa teknolojia ya kidijitali.

Mwelekeo wa shirika

Mfano: Je, Huduma za Utengamao Kidijitali zinalingana na ratiba ya taaluma ya huduma za utengamao? Fikiria muda unaohitajika ili kushughulikia Huduma za Utengamao Kidijitali.

1.6.4 Masharti kwenye kiwango cha mfumo

Kando na masharti ambayo ni lazima yatimizwe na mteja na mtaalamu wa huduma za utengamao, matumizi ya Huduma za Utengamao Kidijitali pia yanategemea muundo wa kisiasa na jamii au/na sheria. Vipengele vifuatavyo vinahushishwa na [34,35].

Fidia kwa Utengamao Kidijitali.

Mfano: Huduma za Utengamao Kidijitali zingewezaje kufidiwa? Fikiria gharama zinazotokea kwa mteja katika ununuzi wa mtandao au teknolojia na sheria zinazofaa katika nchi inayofanya Huduma za Utengamao Kidijitali.

Ufikiaji wa teknolojia/mtandao

Mfano: Je, mteja na mtaalamu wa huduma za utengamao ana uwezo wa kufikia teknolojia au muunganisho ya mtandao unaohitajika ili kutumia Huduma za Utengamao Kidijitali?

Utumiaji wa teknolojia 

Mfano: Je, teknolojia imeundwa ifae watumiaji ili iwezeshe matumizi ya teknolojia?

Ufanisi wa Huduma za Utengamao Kidijitali

Mfano: Kuna uthibitisho wa ufanisi wa uingiliaji kati wa kidijitali?