RADIC

Utengamao kwa wote kupitia ubunifu wa kidijitali na umahiri mpya

person holding a tablet device

Mradi wa RADIC wakamilika kwa mafanikio

Mnamo Tarehe 28 Februari, 2026, Mradi  wa Marekebisho kwa Wote Kupitia Ubunifu wa Kidijitali na Umahiri Mpya [Rehabilitation for All through Digital Innovations and New Comptencies] (RADIC), uliokuwa ukiratibiwa na Chuo Kikuu cha JAMK, ulikamilika na kufungwa rasmi. 

Washiriki wa mradi huu walifanya kazi kwa mashirikiano katika kuimarisha uwezo wa ubunifu wa kidijitali na kuimarisha maendeleo endelevu ya mradi kwa mashirikiano makubwa. Washirki pia walipata nafasi ya kubadilishana taaluma, stadi, maarifa na utatuzi wa changamoto. Pamoja na mambo hayo, mradi huu umeteleta mafanikio makubwa kama vile kutoa vifaa na zana ili kuwasadia walimu, wanafunzi na wadau wengine katika utekelezaji wa kazi zao.

Matokeo ya mradi

Tunafuraha kutangaza matokeo na zana zilizotengenezwa wakati wa mradi wa RADIC sasa zinapatika kwa umma. Zana hizi zinapatikana kwenye tovuti ya  mradi kwa lugha zote mbili ya Kiswahili na Kiengereza.

Zana hizo zina lengo la kuleta mabadiliko ya muda mrefu na kuendeleza  matumizi yake hata baada ya mradi kumalizika ili kusadia ufundishaji na ujifunzaji katika eneo  husika.

Baada ya kuidhinishwa rasmi kwa ripoti ya mwisho ya mradi, matokeo ya RADIC pia yatawekwa kwenye jukwaa la matokeo ya mradi wa Erasmus+  kwa lengo la kuweza kuonekanwa na kufikiwa na hadhira kubwa zaidi.

Shukurani

Kwa namna ya kipekee tunapenda kuwashukuru washirika, wadau wa mradi na wachangiaji kwa kujitoa kwao kwa michango na uwajibikaji, ujuzi wao na mashirikiano yao kwa kipindi chote cha mradi. Juhudi zao thabiti  zimewezesha kufanikisha mradi wa RADIC.

---

RADIC ni kifupi cha maneno “Utengamao kwa wote kupitia ubunifu wa kidijitali na umahiri mpya”. RADIC ni mradi wa utafiti unaolenga kuchangia katika kujenga uwezo wa elimu ya juu ili kusaidia na kuendeleza mabadiliko ya kidijitali katika Afrika Mashariki. Mradi ulianza mwezi Machi 2023 na utaendelea hadi Februari 2026.

"Mradi huu umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya. Maoni na mitazamo iliyotolewa ni ya waandishi pekee na hayaakisi lazima maoni ya Umoja wa Ulaya au Wakala wa Umoja wa Ulaya wa Elimu na Utamaduni (EACEA). Umoja wa Ulaya wala EACEA hawawajibikii maoni hayo."