1.2 Historia

Historia ya Huduma za Utengamao Kidigitali ilianza karne ya 20. Maendeleo katika kompyuta na mawasiliano ya simu yalifungua njia ya mbinu bunifu za utoaji wa huduma za afya, ikijumuisha huduma za utengamao.

Asili na Maendeleo ya Mapema: Huduma za Utengamao Kidijitali zilianza na ujio wa mifumo ya kompyuta na teknolojia za kidijitali zilizojumuishwa katika huduma ya matibabu. Utumiaji wa teknolojia za kidijitali katika huduma za utengamao na matibabu ulianza miaka ya 1980 na 1990. Mfano mmoja wa mapema ulikuwa uundaji wa programu za matibabu zinazosaidiwa na kompyuta kwa ajili ya huduma za utengamao wa neva, hasa kwa wateja walio na kiharusi au matatizo mengine ya neva. Waanzilishi katika uwanja huu walijumuisha Taasisi ya Huduma za Utengamao ya Chicago (sasa Shirley Ryan Ability Lab) ambayo ilianza kutengeneza vifaa vya tiba vinavyosaidiwa na kompyuta kwa ajili ya huduma za utengamao wa kiharusi mapema kama miaka ya 1980. Vifaa hivi viliruhusu wateja kufanya mazoezi yaliyolengwa ili kuregesha au kuboresha ujuzi wao wa viungo vya mwili huku maendeleo yao yakifuatiliwa kidijitali na kurekodiwa. Mfano mwingine wa awali ni matumizi ya teknolojia ya Uhalisia Pepe (UP) katika utengamao. Katika miaka ya 1990, watafiti na matabibu walianza kutengeneza mifumo ya Uhalisia Pepe ili kuunda mazingira ya mtandaoni ambamo wateja walio na hali mbalimbali wangeweza kupata mafunzo na kufanyiwa matibabu. Programu hizi za Uhalisia Pepe zilitumika kwa ajili ya huduma za utengamao wa wateja wa kiharusi, majeraha ya uti wa mgongo, matatizo ya baada ya kiwewe na hali nyinginezo. Ni muhimu kutambua kwamba utumiaji wa teknolojia za kidijitali katika huduma za utengamao na matibabu ni uwanja unaoendelea kubadilika, na watafiti wengi, matabibu, na makampuni yanaendelea kutengeneza teknolojia mpya na za kibunifu ili kuboresha matibabu na kuwapa nafuu wateja.

Maendeleo na Usambazaji (miaka ya 2000 hadi sasa): Katika miongo miwili iliyopita,

Huduma za Utengamao Kidijitali zimebadilika sana. Maendeleo katika Uhalisia Pepe (UP), Uhalisia Ulioboreshwa (UU), robotiki, vihisi na Akili Bandia (AB), yameunda fursa mpya za kuboresha huduma za utengamao. Teknolojia hizi hutumiwa kutengeneza programu za matibabu za kibinafsi zinazolingana na mahitaji ya kibinafsi ya wateja. 

Maono ya baadaye: Huduma za Utengamao Kidijitali zinatarajiwa kuendelea kukua na kuboreka kwani teknolojia kama vile kujifunza mashine na kuchanganua data huwezesha huduma za utengamao na uboreshaji wa programu za matibabu. Kuunganishwa kwa dawasimu na ufuatiliaji wa mbali kutaongeza zaidi ufikiaji na ufanisi wa huduma za utengamao, hasa katika maeneo ya vijijini, au kwa wateja wenye matatizo ya kutembea.