1.1 Upeo
Ukuaji wa kasi wa mtandao na maendeleo katika teknolojia ya kidijitali sio tu kuwa na athari kwa maisha yetu ya kibinafsi, lakini pia ina athari kwa huduma za afya na mfumo wake. Katika miaka ya hivi karibuni, teknolojia za kidijitali zimezidi kutumika katika sekta hii. Teknolojia za kidijitali zinatokana na zana na vifaa vya mitambo ya kompyuta, programu ya kompyuta, na miunganisho. Hii inaweza kujumuisha programu, programu za kompyuta, akili bandia lakini pia vifaa kama simu janja, vipakatilishi na vitarakilishi na vinginevyo vingi. Kwa habari zaidi, angalia sura ya 6 “Teknolojia”.
Tunapojumuisha teknolojia za kidijitali katika huduma za utengamao, tunaita Huduma za Utengamao Kidijitali. Neno “Huduma za Utengamao Kidijitali” bado halijatumika sana. Huduma za Utengamao Kidijitali zinaweza kuchanganywa na neno dijitali afya na kuchukuliwa kama kisawe. Hata hivyo, Huduma za Utengamao Kidijitali si sawa na dijitali afya ingawa kunaweza kuwa na mwingiliano fulani. Tunafafanua Huduma za Utengamao Kidijitali kama uingiliaji kati wa kutumia zana za kidijitali, teknolojia, na huduma ili kuboresha utendakazi, kupunguza ulemavu, kufuatilia, na kutathmini afya ya watu walio na matatizo ya kiafya. Huduma za Utengamao Kidijitali kwa hivyo ni neno pana ambalo linamaanisha sio tu zana zinazotumika katika huduma za utengamao; bali linalenga kuwezesha mchakato wa kidijitali. Teknolojia za kidijitali zina matumizi mengi yanayowezekana katika mfumo wa huduma ya afya. Kwa mfano, zinaweza kutumiwa katika usimamizi wa safari ya mteja katika sekta ya afya k.m fikiria usajili katika mtoa huduma ya afya na/au kwa ajili ya huduma za utengamao wa wateja kama vile [1]. Katika mchoro 1, unaweza kuona uwezekano wa matumizi mbalimbali ya Huduma za Utengamao Kidijitali wakati wa safari ya mteja.

Mchoro wa 1: Matumizi ya Huduma za Utengamao Kidijitali katika sekta ya afya.
Uamuzi wa kutumia Huduma Utengamao Kidijitali daima unategemea mahitaji ya mteja ili kuboresha matokeo ya huduma hizi, kupunguza ulemavu na kuiwezesha jamii na mteja. Uamuzi huo unazingatia maisha ya kila siku ya mteja na chaguzi anazofanya. Mtaalamu wa afya na mteja huchukua kwa pamoja uamuzi wa kujumuisha teknolojia za kidijitali katika huduma za utengamao.
Katika Huduma za Utengamao Kidijitali, mchakato wa huduma hizi unaweza kuwa zaidi ya shughuli zinazohusiana na uwepo wa mtaalamu wa huduma ya afya, mwongozo wa kitamaduni na mahali. Katika ubora wake, unaweza kujumuisha kwa urahisi udhibiti wa kibinafsi wa huduma za utengamao unaoongozwa na mtaalamu wa huduma ya afya. Huduma za kidijitali hazichukui nafasi ya wataalamu wa afya wenye uwezo, lakini mchanganyiko huo unaweza kutoa manufaa mengi kwa mteja, mtaalamu wa afya na kwa mfumo wa huduma ya afya.