2.1 Mbinu bora kutoka Uganda, Zambia, na Ethiopia
Taasisi shirika za muungano wa RADIC ziko Kenya, Tanzania, Zanzibar, na Rwanda. Katika nchi hizi, matatizo ya kawaida ya kiafya ni kiharusi, VVU na kifua kikuu (KK) [7]. Huduma za utengamao ni muhimu kwa kushughulikia mahitaji ya kimwili, kiakili, na kisaikolojia ya watu wanaoishi na kiharusi, VVU, na kifua kikuu kukuza uhuru wao wa utendaji, na kuboresha ustawi wao kwa ujumla. Katika nchi zote tatu, mahitaji ya huduma za utengamao wa kiharusi, VVU na kifua kikuu yanazidishwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na upatikanaji haba wa vituo vya huduma za afya, uhaba wa wataalamu waliohitimu, uhaba wa kufadhili programu za huduma za utengamao na unyanyapaa wa kijamii kwa watu walio na hali hizi. Kuzieleza changamoto hizi na kuboresha ufikiaji wa huduma kamili za utengamao ni muhimu katika kupunguza ulemavu, kukuza afueni ya utendaji kazi, na kuimarisha matokeo ya jumla ya afya ya watu walioathirika na VVU, KK, na kiharusi nchini Kenya, Tanzania, Zanzibar na Rwanda.
Kwa sababu hii, tungependa kuwasilisha mifano mitatu ya mbinu bora ambapo Huduma za Utengamao Kidijitali hutumika kuongeza hatua ya ufikiaji wa huduma hizi, kuunda jumuiya ya rika bila kunyanyapaliwa, kuboresha uzingatiaji wa tiba na kupunguza gharama za huduma za utengamao.
Kumbuka: Uingiliaji kati wa Huduma za Utengamao Kidijitali unaweza pia kutumika katika maeneo mengine yaliyofafanuliwa katika mifano hii. Hiyo ina maana kwamba uingiliaji kati wa Huduma za Utengamao Kidijitali pia unaweza kutumika kutathmini, kuchunguza, kama uingiliaji kati, kufuatilia hali/dalili za mteja na kutathmini matokeo ya huduma za utengamao. Tazama sura ya 1 na/au 6 kwa habari zaidi.
Mbinu bora nambari 1:
Mfano wa kwanza wa mbinu bora unatokana na uchapishaji kutoka kwa Terio na wengineo na Kamwesiga na wengineo [8,9].
Uingiliaji kati wa simu janja husaidia kuboresha ufikiaji wa Huduma za Utengamao- Uchunguzi Kifani kutoka Uganda.
Changamoto
Kuenea kwa ugonjwa wa kiharusi nchini Uganda kunaongezeka. Licha ya kuongezeka kwa mzigo wa magonjwa, nchi haina mikakati au programu za kitaifa za kuzuia au kutibu magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kiharusi.
Nchini Uganda, 72% ya vijiji vinaishi ndani ya kilomita tano kutoka kituo cha afya. Hata hivyo, utumiaji wa vifaa ni mdogo kutokana na sababu kama vile ukosefu wa usafiri, miundombinu duni, ukosefu wa wafanyakazi na ukosefu wa kuwamotisha wafanyakazi. Huduma ya matibabu hutolewa katika ngazi maalumu ya elimu ya juu na Hospitali za Rufaa za Kitaifa, kama vile Hospitali ya Mulago katika mji mkuu wa Kampala, ambapo watu walio na kiharusi hulazwa. Huduma ya pili hutolewa na Hospitali za Rufaa za Mikoa, ambazo zina wataalamu haba. Huduma za kimsingi hutolewa na huduma za afya katika jamii, ambapo uwezo wa huduma hutofautiana. Sekta ya afya ya kibinafsi inawajibika kwa karibu 50% ya huduma za afya.
Fursa
Matumizi ya dijitali yanakua katika Kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika. Kwa sasa kuna zaidi ya huduma 1000 za afya ya simu katika nchi zenye mapato ya chini zinazochunguza na kutoa huduma za afya. Lengo moja la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ni kulenga maisha yenye afya na kukuza ustawi kwa wote. Kutokana na hali hii, matumizi ya simu za mkononi yanaweza kuongeza ubora, kupunguza gharama, na kupanua ufikiaji wa huduma za afya kwa manufaa ya mamilioni ya watu. Katika nchi za Kiafrika, matumizi ya simu janja yamekubalika kwa haraka. Mwaka 2017, katika Kusini mwa Jangwa la Sahara , watu milioni 444 walikuwa na usajili wa simu za mkononi. Mtandao mpana wa simu sasa unashughulikia maeneo mengi ya mijini, ikimaanisha kuwa kutengwa kwa uhusiano na miundombinu ni kwingi zaidi katika maeneo ya vijijini. Nchini Uganda, matumizi ya simu janja yameongezeka polepole kote nchini tangu 1995 na mnamo 2017, idadi ya miunganisho ya simu janja ilikuwa 58 kwa kila wakazi 100.
Hii inaonyesha kuwa kuna uwezekano wa ufanisi wa matumizi ya simu za mkononi ili kuboresha ufikiaji wa huduma za afya, hasa kutokana na ongezeko la mahitaji ya kijamii katika matumizi ya teknolojia katika shughuli za kila siku. Uwezo wa kutumia teknolojia za dijitali ukijumuisha suluhu za simu za rununu kwa walionusurika na kiharusi tayari umeripotiwa.
Suluhisho
Uingiliaji kati wa U@so ulitekelezwa nchini Uganda mwaka wa 2016 na unalenga kuongeza utendaji katika shughuli za kila siku kwa watu wanaoishi na matokeo ya kiharusi, pamoja na watu hao kushiriki katika maisha ya kila siku na wanafamilia wao.
Maelezo mafupi ya wateja ambao wanaweza kufaidika na uingiliaji kati wa U@so
- Watu wazima wenye kiharusi
- Watu wanaoishi katika sehemu ya mashambani mwa Uganda
- Ufikiaji na uwezo wa kutumia simu ya mkononi
- Mwanafamilia au mlezi aliye tayari kumsaidia mteja
Katika uingiliaji kati wa U@so, U inasimamia (Uso kwa uso kati ya Mtaalamu wa Kazi (MK) na mteja), @angalia, S Shirikiana na O Ona. Katika uingiliaji kati wa U@so, vipengele vya kidijitali huunganishwa na vipindi vya ana kwa ana. Wakati wa uingiliaji kati, malengo matatu yaliyowekwa ya shughuli yalipaswa kuwasilishwa kwa mteja kila asubuhi na jioni kwa huduma ya arafa. Arafa ya asubuhi ilikuwa ukumbusho wa kufanya shughuli wakati wa mchana. Jioni, mteja alitakiwa kujibu kwa arafa tatu tofauti kwa kufunga utendaji wa shughuli kati ya 0 (hajafanya shughuli) na 5 (alifanya shughuli vizuri). Iwapo wateja wamepata alama 0 au hawakujibu arafa, bendera nyekundu (ujumbe unaoarifu kuhusu shughuli isiyotekelezwa) ilitumwa kwa MK ambaye angempigia simu mteja asubuhi iliyofuata ili kutatua tatizo. Zaidi ya hayo, wateja walipaswa kupokea simu za ufuatiliaji kutoka kwa MK mara mbili kwa wiki.
Ufuatiliaji na ukumbushaji teknolojia
- Wateja hutumia simu ya mkononi ya kawaida kupokea ukumbusho, simu na kutuma arafa/ujumbe.
- Ujuzi mdogo wa mtandao unahitajika ili kupokea na kutuma ujumbe.
- Kwa mtaalamu wa huduma za utengamao, ujumbe hutumika kama chombo cha kufuatilia huduma za utengamao na kutambua mianya ya utendaji ili kusaidia kuziba mapengo hayo.
Sifa kuu bainifu za uingiliaji kati wa U@so
- Uingiliaji kati uliochanganywa, kuhusisha kikao cha uso kwa uso na sehemu za mtandaoni.
- Uingiliaji kati hulengwa kulingana na mahitaji ya wateja ili kuboresha utendajikazi wa shughuli za maisha ya kila siku.
- Kuhusisha wanafamilia wa watu wengine muhimu.
- Kuunda malengo matatu ya uingiliaji kati yanayoweza kuhamishwa kwa mazingira ya nyumbani katika shughuli za kila siku.
- Wanafamilia hujulishwa kuhusu shughuli zinazolengwa na wateja na mikakati inayopangwa ya kufikia malengo haya.
- Kutumia matokeo ya mteja ili kufuatilia na kutathmini huduma za utengamao.
- Huwezesha mabadiliko kupitia kuweka malengo na kuunda mikakati kwenye wavuti ya U@so.
Athari za uingiliaji kati wa U@so
- Uingiliaji kati unaweza kuongeza ufikiaji, uwezeshaji, na uendelezaji katika mchakato wa huduma za utengamao baada ya kiharusi lakini katika eneo hili bado kuna ukosefu wa utafiti.
- U@so inaonekana kukubalika kwa wateja na wanafamilia.
- Dalili zaonesha kwamba uingiliaji kati huongeza utendajikazi na kujitegemea katika maisha ya kila siku.
Changamoto zinazokabiliwa wakati wa utekelezaji
- Ukosefu wa ushirikiano kati ya wafanyakazi wenzake au wafanyakazi wengine wa matibabu.
- Kutowajibika kwa wateja na wanafamilia.
- Kutoamini jinsi uingiliaji kati ulivyo na manufaa.
- Kuharibika kwa seva kinyume cha matarajio/matatizo ya kiufundi.
- Ukosefu wa maarifa kuhusu utendajikazi wa teknolojia.
- Ukosefu wa elimu ya dijitali afya.
Ujumbe muhimu wa utekelezaji
- Huduma zinahitaji kuunganishwa kwa uangalifu katika muktadha wa kiasili.
- Majukumu tofauti katika ngazi mbalimbali katika utekelezaji yanahitajika, hivyo basi kuimarisha utamaduni wa kufanya kazi unaosaidia.
- Wataalamu wa huduma za utengamao na wateja waliotiwa motisha kuwa kama wawezeshaji.
- Uongozi wenye uwezo→ wawezeshaji kuandaa warsha zenye mijadala ya wazi isiyo ya kitabaka.
- Motisha kwa wateja na wataalamu wa huduma za utengamao inaweza kuongezwa kupitia motisha za kifedha.
- Taarifa kuhusu manufaa ya uvumbuzi inapaswa kutolewa kwa wateja na wanafamilia kabla ya uingiliaji kati.
- Utafiti zaidi wenye sampuli kubwa unahitajika ili kuthibitisha ufanisi wa uingiliaji kati.
Mbinu bora nambari 2:
Mfano wa pili wa mbinu bora unatokana na uchapishaji kutoka kwa Simpson na wengineo [10].
Kuunda jumuiya yenye vikundi vya usaidizi wa kidijitali kwa wanawake wajawazito wenye umri mdogo wanaoishi na VVU: Mbinu bora za utendaji kutoka Zambia
Changamoto
Upimaji wa mara kwa mara wa VVU wakati wa ujauzito kwa wanawake vijana mara nyingi huwa ni kujifunza hali zao za VVU kwa mara ya kwanza. Ingawa hii imeboresha kwa kiasi kikubwa matibabu ya kurefusha maisha (KM) nchini Afrika ya Kusini, vijana wajawazito wanakabiliwa na changamoto za kupata huduma za VVU na kuna uwezekano mdogo wa kuzitumia. Wale walio na VVU kabla au wakati wa ujauzito wana uwezo mkubwa wa kutofuata KM. Unyanyapaa wakati wa ujauzito, pamoja na kudhibiti VVU na uzazi, kunaweza kuathiri vibaya afya ya uzazi na ukuaji wa mtoto. Wasiwasi kuhusu hali ya VVU na upimaji inaongeza msongo wa mawazo kwa wajawazito.
Fursa
Uboreshaji wa usaidizi wa kijamii umeonyeshwa kuwa na matokeo chanya katika ufuasi wa dawa katika magonjwa sugu anuwai kwa watu walio katika mazingira magumu. Kuna ushahidi wa kupendekeza kwamba vikundi vya usaidizi na ushauri rika ni uingiliaji kati madhubuti wa kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wajawazito wanaoishi na VVU. Pale ambapo pana vizuizi vikubwa vya kuhudhuria ushauri wa ana kwa ana au vikundi vya usaidizi- uingiliaji kati wa kiteknolojia una nafasi muhimu. Uingiliaji kati unaotegemea simu za rununu unaweza kushinda vizuizi ambavyo watu lazima wapate usaidizi muhimu wa kijamii na kisaikolojia. Simu za rununu zinaweza kutumika kama chombo cha kuelimisha, na katika uwezo huo kama kifaa cha mabadiliko ya tabia na usaidizi wa kisaikolojia kwa watu wanaoishi na VVU.
Suluhisho
Vikundi vya usaidizi rika vinavyotokana na simu za rununu vilianzishwa nchini Zambia mwaka 2018. Lengo la vikundi hivyo vya usaidizi lilikuwa kukabiliana na athari mbaya za kutengwa na jamii na unyanyapaa wa afya ya akili ambao watu wengi walioambukizwa VVU wanakabiliwa nayo.
Sifa bainifu zilizoidhinishwa nchini Zambia
- Mahitaji ya huduma ya afya katika kila jamii yanahudumiwa na kliniki moja ya serikali, ambayo hutoa huduma za ndani na nje kwa mteja. Vituo vya afya hapo awali viliundwa kwa ajili ya watu wachache, lakini kutokana na uhamiaji wa watu kutoka vijijini kwenda mijini na kuundwa kwa makazi yasiyo rasmi, idadi ya watu na maeneo yanayohudumiwa na vituo vya afya vya serikali za mitaa yameongezeka.
- Wastani wa maambukizi ya VVU katika jamii ambapo uingiliaji kati ulianzishwa ni 12%.
Maelezo mafupi ya mteja ambaye angeweza kufaidika kutokana na uingiliaji kati
- Wanawake wajawazito wenye VVU.
- Ufikiaji na uwezo wa kutumia simu ya mkononi.
- Wanawake wanaotaka kupata huduma za VVU bila hofu ya kunyanyapaliwa.
Sifa kuu bainifu za kikundi cha usaidizi-rika dijitali.
- Kikundi cha usaidizi-rika kinajumuisha wateja 6-8 na usaidizi huo ulidumu kwa miezi 4 katika kipindi cha kabla na baada ya kujifungua.
- Vikundi vya kidijitali vinaundwa kupitia rocket. Chat ® .
- Rocket.Chat® inahakikisha usiri na kutojulikana kwa watumiaji.
- Wateja wanaweza kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe kwa uhuru bila kujulikana.
- Msimamizi mmoja aliyefunzwa anafuatilia mazungumzo.
- Vikundi vya usaidizi rika vinaweza kutumiwa kupitia simu janja (vifaa vya rununu vya ITEL 1503, vinavyotumia mfumo wa uendeshaji wa kitkat® wa Android 4.4).
- Mada zinazojadiliwa katika kikundi cha usaidizi rika hulenga msaada wa kijamii na mahusiano, unyanyapaa, VVU, maarifa na ufuasi wa dawa.
- Vikao vya kawaida vya kidijitali na mtaalamu wa afya hufanyika ili kushughulikia maswali mahususi ya matibabu kutoka kwa wateja.
Utekelezaji
Wakati wa uzinduzi, wateja walipewa kifaa cha rununu chenye data iliyopakiwa. Waliambiwa wachague jina la utani na kubaki bila majina yao wakati wa uingiliaji kati. Walihimizwa kuweka maudhui kwa siri na wasipeane simu zao. Vikundi vya usaidizi vilitumia teknolojia ya chanzo huria, rocket. Chat ®. Mfumo huu ulihakikisha kuwa wateja hawawezi kupeana nambari, kusambaza jumbe, kupiga au kutuma picha au video. Timu inaweza kusimamia vikundi hivyo na kufuatilia mazungumzo.
Vikundi vilishughulikiwa na Mshauri Rika aliyefunzwa ambaye aliwasilisha mada za mtaala ulioandaliwa kwa kushauriana na timu ya mradi na wadau. Kulikuwa na vikao ambapo wataalamu wa afya-mwana jinakolojia, mtaalamu wa lishe, na mtaalamu wa jumla- walialikwa katika vikundi ili kuendesha kipindi kuhusu mada fulani, ambapo wateja wangeweza kuuliza maswali mahususi. Mwishoni mwa vikundi, wateja waliombwa kuhifadhi simu zao, lakini ujumbe huo ulifutwa katika simu zao ili kuzuia wasiwasi wa maadili na habari kuhusu mazungumzo ambayo hayakufuatiliwa au hayakushughulikiwa.
Changamoto wakati wa utekelezaji
- Mvutano na mashirika ya wanawake juu ya ushiriki wao katika mradi.
- Stadi duni za wateja za kusoma na kuandika.
- Matatizo ya kiufundi/marekebisho ya simu: wateja walivunjwa moyo wakati ''simu zilipochelewa kurudishwa wakati zilipoenda kurekebishwa''.
- Sio vikundi vyote vilikuwa na washughulikiaji waliochangamka, ambapo ilisababisha mada kubaki juu juu.
Ujumbe muhimu wa utekelezaji.
- Wateja waliweza kutumia jukwaa, hata kama viwango vyao vya kusoma na kuandika au stadi ya lugha ya Kiingereza vilikuwa chini. Utendajikazi wa kukagua tahajia-kwa-maandishi uliwezesha hali hiyo ya mtagusano.
- Kutokubaliana kwa uingiliaji kati kilikuwa kipengele muhimu cha kutumia kikundi cha usaidizi-rika.
- Muundo unaoongozwa na vikundi vya usaidizi rika wa kijamii ulikuwa ni jambo muhimu la kukubalika kwani ulihimiza nafasi ya kidemokrasia na isiyo na hofu kwa wanawake.
- Muundo na urafiki wa mtumiaji wa simu hufanya matumizi ya uingiliaji kati kuwa rahisi.
- Huduma za uso kwa uso lazima ziundwe ili kupongeza utoaji wa kidijitali ili wale ambao hawawezi kushiriki katika uingiliaji kati kama huo waweze kuhudumiwa vyema.
- Idadi ya watu pia iko katika hatari kubwa ya Unyanyasaji wa Wapenzi wa Karibu. Nchini Zambia, 43% ya wanawake wenye umri wa miaka 15-49 waliripoti uzoefu wa maisha ya kimwili na/au kingono UWK (Unyanyasaji wa Wapenzi wa Karibu) na 27% ya wanawake waliripoti UWK ya kimwili na/au kingono (Unyanyasaji wa Wapenzi wa Karibu) katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. Kuanzishwa kwa simu za rununu katika mazingira hatari kama haya kunaweza kusababisha wivu au mashaka, kubadilisha mitazamo katika vijiji. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba timu ya wataalamu iliyofunzwa inaweza kushirikisha washirika au wanafamilia wengine katika mchakato wa idhini ili kulinda wateja.
Mbinu bora nambari 3:
Mfano wa tatu wa mbinu bora unatokana na uchapishaji kutoka kwa Manyazewel na wengineo. [11-13].
Kichunguzi Kikumbusho dawa za kidijitali hupunguza gharama za huduma ya afya kwa watu walio na kifua kikuu: Uchunguzi kifani kutoka Ethiopia.
Changamoto
Ugonjwa wa Kifua Kikuu bado unapatikana zaidi katika maeneo maskini na huathiri watu ambao hawana pesa nyingi . Dawa zinazotumika kutibu KK hufanya kazi vizuri, lakini ni ghali kwa wateja na familia zao kwa sababu lazima waende sehemu maalum kupata dawa. Hii inafanya iwe vigumu kwao kushikamana na mpango wa matibabu, na wakati mwingine matibabu hayafanyi kazi, na kusababisha vijidudu vya KK kuwa sugu kwa dawa. Hii inaweza kufanya ugonjwa kuenea kwa watu wengine. Matibabu ya sasa ya KK hudumu kwa muda mrefu, angalau miezi sita kwa KK ya kawaida na hata zaidi kwa KK sugu ya dawa. Katika maeneo mengi, wateja lazima waende kliniki kila siku kuchukua dawa zao chini ya uangalizi wa mhudumu wa afya. Hii inakuwa vigumu kwa wateja na familia zao kwa sababu lazima watumie pesa nyingi kwa usafiri, chakula, na mahali pa kukaa karibu na kliniki.
Fursa
Kichunguzi Kikumbusho Dawa (KKD) ni kifaa cha kidijitali ambacho hufuatilia matibabu kwa wagonjwa wa kifua kikuu kinachoweza kushughulikia masuala haya. Kifaa cha KKD (Teknolojia za Wisepill) kinajumuisha moduli ya kielektroniki na chombo cha dawa cha kurekodi uzingatiaji, uhifadhi dawa, utoaji tahadhari unazosikika na ishara za mwanga zinazoonekana zenye rangi (yaani, kijani kibichi, manjano na nyekundu) ili kuwakumbusha wateja kumeza na kujaza tena dawa zao, na kuruhusu madaktari kufuatilia uzingatiaji wao kidijitali.
Suluhisho
Usambazaji wa dawa za siku 15 za KK (tiba ya mchanganyiko wa HRZEya dozi 15) katika kifaa cha kielektroniki cha ufuatiliaji na ukumbusho wa dawa za kidijitali (evriMed500 kifaa cha kidijitali cha kifuatilia na kukumbusha matumizi ya dawa kilichotengenezwa na wisepill Technologies, Afrika Kusini) ili kujisimamia, tazama picha hapa chini. Uingiliaji kati ulianzishwa mwaka 2020 nchini Ethiopia ili kupunguza gharama za usafiri na kuboresha uzingatiaji wa tiba kwa wateja wenye Kifua Kikuu.

Figure 1: evriMed500, Kichunguzi Kikumbusho Dawa
Maelezo mafupi ya wateja ambao wanaweza kufaidika kutokana na uingiliaji kati
- Watu wenye umri zaidi ya miaka 18 wenye Kifua Kikuu.
- Hali ya mteja akiwa nje ya kliniki.
- Watu wasioishi karibu na kliniki ya KK.
- Idhinishwa kufuata tiba ya miezi 2 ya dawa ya KK iliyopendekezwa na WHO (Shirika la Afya Ulimwenguni) [14].
Sifa kuu bainifu za uingiliaji kati.
- Kichunguzi Kikumbusho Dawa cha kidijitali (kifaa cha KKD, tazama picha 1) kilitolewa kwa wateja na dozi 15 za dawa katika kliniki ya KK.
- Wateja wanaweza kurudi nyumbani kwa siku 15 zijazo.
- Kifaa kina viashiria vitatu vya kutoa mwangaza vinavyoonekana kupitia sehemu ya mbele ya chombo kwa ajili ya ukumbusho wa kila siku wa dawa (mwanga wa kijani), ukumbusho wa kujaza dawa, (mwanga wa manjano), na arifa za betri ya chini (mwanga mwekundu). Pia kina mvumo ambao huwashwa wakati wa mfuatano wa kengele, na hutoa sauti laini wakati chombo kinafunguliwa au kufungwa.
- Baada ya siku 15, wateja wanarudi kliniki ya KK, ambapo wanahesabu vidonge vilivyosalia kwenye kisanduku cha vidonge, kupakua data ya kumeza kutoka katika kifaa, kutathmini utendajikazi wa kifaa na kusuluhisha inavyohitajika, na kufanya upimaji wa mkojo.
- Wateja wanaweza kushauriana na mtoa huduma ya afya iwapo atakuwa na hali ya ugonjwa wa kimatibabu au matukio yoyote mabaya kando ya ziara iliyoratibiwa kabla ya muda unaofuata.
- Nambari ya simu ya mtoa huduma ya afya kufuatia hali ya mgonjwa wa KK itaandikwa nyuma ya kadi zao za miadi.
Utekelezaji
- Wateja waliarifiwa jinsi ya kutumia kifaa na kupewa kijikaratasi chenye maelezo mazuri ya mteja kilichotayarishwa kwa lugha ya taifa ambacho kilieleza taratibu za kufuata.
- Wateja walipokea dawa za KK za muda wa siku 15 (HRZE matibabu mchanganyiko ya kipimo kisichobadilika cha dozi 15) katika kifaa cha KKD ili kujihudumia.
- Wateja walirudi kliniki kila baada ya siku 15, wakati ambapo daktari alihesabu vidonge vilivyosalia kwenye kisanduku cha vidonge na kuunganisha moduli ya KKD na kompyuta.
- Daktari pamoja na mteja alipakua data ya kuchukua vidonge kutoka kwa kifaa hadi kwenye kompyuta na kukagua ripoti za matukio katika siku 15 zilizopita. Tukio lolote ambalo halikufanyika kuhusu maelezo ya kutumia katika muda uliowekwa katika ripoti ya tukio lilitathminiwa dhidi ya vidonge vyovyote vilivyosalia kwenye kisanduku cha vidonge na kujadiliwa zaidi na mteja kwa uthibitisho.
Ujumbe muhimu kwa utekelezaji
- Uwezo wa kutumia kifaa cha KKD ulikuwa wa juu.
- Wateja waliotumia kifaa cha KKD walitembelea kituo cha huduma ya afya kila baada ya siku 15 na hii ilipunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa wateja kuwa na vikwazo vya msingi ikiwa ni pamoja na gharama za usafiri, chakula na malazi katika ziara za kibinafsi za kila siku.
- Kliniki za KK katika utafiti tayari zilikuwa na kompyuta zinazotumika kabla ya utafiti. Programu ya KKD ilianzishwa kwenye kompyuta ambazo tayari zilikuwa zinatumika katika kliniki za KK au maeneo kama hivyo.